Tangazo hilo lilitolewa na dadake mkubwa Raila, Ruth Odinga, ambaye alifichua kwamba Beryl alifariki Jumanne, Novemba 25.
Hata hivyo, hakufichua sababu ya kifo hicho.Huku akithibitisha kufariki kwa Beryl, Ruth alifichua kuwa Achieng alikuwa bintiye mke wa kwanza wa Jaramogi, Mary Auma na dadake Raila Odinga na Oburu Oginga.