Huku idara ya polisi ikitarajiwa kuanza zoezi la kuwasajili maafisa wapya wa polisi kuanzia hapo kesho, onyo kali limetolewa kwa wale watakaopatikana wakitoa au kupokea hongo katika shughuli hiyo ya uajiri.

Akizungumza na wanahabari inspekta generali wa polisi Douglas Kanja amesema kwamba shughuli hiyo itaendeshwa kwa uwazi na haki huku akitoa wito kwa umma kuripoti visa vya ufisadi

Idara ya polisi inalenga kuwasajili maafisa wapya alfu kumi, uzinduzi huo ukiashiria mwanzo wa mchakato wa uajiri wa siku tano ambao kwa mara ya kwanza utaendeshwa kwa ushirikiano na tume ya polisi ipoa pamoja na mashirika mengine.