You are currently viewing HARAMBEE STARLETS KWENYE HARAKATI MPYA

HARAMBEE STARLETS KWENYE HARAKATI MPYA

Timu ya taifa ya kandanda ya wanawake, Harambee Starlets, itamenyana na ushelisheli leo hii katika raundi ya kwanza ya mechi za kufuzu kwa michezo ya Olimpiki ya mwaka 2028.

Ingawa ni mechi ya ugenini kwa Kenya, lakini Ushelisheli imewakaribisha wakenya katika uwanja wa michezo wa Ulinzi jijini Nairobi hapa nchini Kenya.

Hii ni mechi ya kwanza ya kocha mkuu Godfrey Solo Oduor, ambaye aliteuliwa wiki iliyopita kuchukua nafasi ya Beldin Odemba ambaye alijiuzulu.

Kocha Oduor ana wachezaji 25 wa kuchagua katika mechi mbili zitakazo chezwa katika muda wa wiki moja kwenye uwanja huo mmoja.

Timu hiyo imemkaribisha beki Janet Mumo na viungo Korazon Oquino na Sheril Angach ambao hawajakuwepo kwa sababu mbalimbali. Kocha Solo anasema, atatumia wachezaji tofauti kwa mechi hizo.

APERIT FM, HII NI YETU