You are currently viewing IDARA YA UTALII NA WANYAPORI YAKANUSHA KAULI YA GACHAGUA

IDARA YA UTALII NA WANYAPORI YAKANUSHA KAULI YA GACHAGUA

Wizara ya Utalii na wanyama pori, imeyakosoa matamshishi ya kiongozi wa chama cha DCP Rigathi Gachagua, aliye wataka watalii na wawekezaji wa kigeni kuahirisha safari zao za kuja hapa nchini kutokana na madai ya kuzorota kwa usalama.

Katika taarifa yake katibu wa Idara ya Utalii Julias Bitok, amesema kauli hizo zinaweza kuathiri sekta ya utalii, kupunguza imani ya wawekezaji na kuhatarisha ajira ya maelfu ya wakenya, wanaotegemea sekta hiyo kujipatia riziki.

Katibu Bitok amesema Kenya iliwapokea watalii wa kimataifa takriban milioni 2.7 mwaka jana, uku serikali ikilenga kuongeza idadi hiyo hadi milioni 5 ifikapo mwaka wa 2028.

Kauli ya bitok inajiri kufuatia kauli ya gachagua jumapili iliyopita, akiwa katika kaunti ya Kirinyanga akiwataka watalii na wawekezaji, kusubiri hadi baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027, kabla ya kuzuru au kuwekeza hapa nchini, akidai kuwa hali ya usalama nchini Kenya ni ya kutilia shaka.

Hata hivyo msemaji wa serikali Isaac Mwaura, amepinga kauli ya Gachagua akisistiza kuwa Kenya ni salama kwa watalii na wawekezaji.