Wizara ya utalii imetangaza kiingilio cha bure katika mbuga, hifadhi na maeneo ya akiba yote ya kitaifa yanayosimamiwa na shirika la huduma ya wanyamapori kws, siku ya jumamosi, septemba tarehe 27,
katika taarifa yake, waziri wa utalii, Rebecca Miano, amesema serikali ya Kenya inatoa ruhusa hii kwa raia wote wa kenya kuadhimisha siku ya utalii duniani ya umoja wa mataifa.
Miano ameongeza kuwa mpango huo unalenga kuwapa wakenya fursa ya kuungana tena na urithi wa wanyamapori, kuimarisha jitihada za uhifadhi, na kufurahia uzuri wa hazina asilia nchini.
Siku ya Utalii Duniani huadhimishwa kila mwaka septemba 27, na kauli ya mwaka huu ni ‘utalii na mabadiliko endelevu,’ ikisisitiza mchango wa utalii katika jamii, uhifadhi na ukuaji wa uchumi.