You are currently viewing KIPCHOGE ASHINDA MARATHONI KWA MARA YA KWANZA TANGU 2023

KIPCHOGE ASHINDA MARATHONI KWA MARA YA KWANZA TANGU 2023

Eliud Kipchoge ameshinda marathoni ya Melbourne, ushindi wake wa kwanza tangu Berlin mwaka 2023. Nyota huyo amevunja rekodi ya mbio hizo katika ziara yake ya mabara saba ya kuchangisha fedha kwa shughuli za kijamii.

Eliud Kipchoge atwaa ushindi Melbourne baada ya miaka mitatuMwanariadha nyota wa Kenya, Eliud Kipchoge, ameshinda marathoni ya Melbourne nchini Australia leo Jumapili, ukiwa ushindi wake wa kwanza katika mbio za marathoni tangu Berlin mwaka 2023.

Bingwa huyo wa Olimpiki mara mbili amemaliza mbio kwa saa mbili, dakika tisa na sekunde kumi, akivunja rekodi ya mbio hizo kwa sekunde mbili.

Kipchoge alijitenga na wapinzani wake katika kilomita kumi za mwisho, kabla ya kufika kwenye mstari wa mwisho ndani ya uwanja maarufu wa kriketi wa Melbourne. Sehemu ya mbio hizo ilipitia kwenye njia inayotumika kwa mashindano ya magari ya Formula One katika eneo la Albert Park.

Kipchoge amesema alifurahia mashabiki waliokuwa wakimshangilia na kuita jina lake. Ameongeza kuwa anajivunia kukimbia pamoja na kizazi kipya na kuhamasisha wakimbiaji wa Melbourne.

Mbio hizo ni sehemu ya mpango wake wa kukimbia marathoni katika mabara yote saba, likiwemo Antaktika, ndani ya miaka miwili, ili kuchangisha fedha kwa shughuli anazoziunga mkono.

Melbourne ilikuwa kituo chake cha tatu, baada ya Afrika Kusini na Brazil. Mwaustralia Thomas Do Canto ameshika nafasi ya pili, huku Camille French wa New Zealand akishinda mbio za wanawake.