Agizo la rais William Ruto kuondoa marufuku ya kukata miti, imepokelewa kwa hisia mseto na maseremala, wafanyikazi wa viwanda vya kupasua mbao katika kaunti ya transnzoia.
Maseremala wametaja agizo hilo kuwa afueni hasa ikizingatiwa kuwa, wafanyikazi wengi waliachishwa kazi na kuongeza kwamba imekuwa ngumu kupata kandarasi ya kutengeneza fanicha katika afisi za serikali.
Kwa upande wao wauza mbao mjini Kitale wanasema biashara yao imedorora kutokana na wateja kukumbatia bidhaa vinavyo tengenezwa kwa plastiki na vyuma.
Hivi majuzi rais Wiliam Ruto aliondoa marufuku ya ukataji miti ili kuruhusu uvunaji wa miti iliyokomaa katika misitu kote nchini, akisema hatua hiyo inalenga kukuza viwanda vya ndani na kupunguza utegemezi wa bidhaa za mbao zinazoagizwa kutoka nje.