Kaunti ndogo za Pokot ya Kati na Pokot Kaskazini ndizo zinaongoza katika viwango vya ukeketaji katika kaunti ya Pokot Magharibi.
Kwa mujibu wa mkurugenzi katika idara ya jinsia katika kaunti hiyo Emmanuel Oigo,viwango hivyo hata hivyo vimepungua kutoka asili mia 72 hadi 44 katika kaunti.
Akizungumza katika warsha ya mafunzo kwa wahabari mjini Kapenguria,afisa huyo amebaini kwamba,kwa sasa taifa limerekodi asili mia 15 ya visa vya ukeketaji nchini.
Katika kaunti ya Pokot magharibi,vsa vya ukeketaji vimechangiwa na utamaduni uliopitwa na wakati miongoni mwa jami ya wafugaji
Wakati huohuo,Mkurugenzi wa Kituo cha Kuimarisha Demokrasia na Utawala Bora (CEDGG), Paul Masese, amewatahadharisha wahudumu wa afya wanaojihusisha na ukeketaji kwamba,hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Akizungumza baada ya kukamilika kwa warsa hiyo,mratibu wa baraza la vyombo vya habari ukanda wa bonde la ufa Joseph Mecha,amewatolea mwito wanahabari kutumia majukwaa yao ipasavyo na kuripoti habari zitakazosaidia katika kupambana na mila zilizopitwa na wakati.
