Mbunge wa Kesses Julius Rutto amesema vyama vya upinzani nchini havina msimamo wa pamoja kuhusu sababu inayowasukuma kuungana, akidai kuwa kila upande unaonekana kuwa na malengo yake katika ushirikiano huo.
Rutto amesema ingawa viongozi wa upinzani wamekuwa wakifanya mikutano na kuzungumzia uwezekano wa kushirikiana kisiasa, bado hawajaweka wazi ajenda ya pamoja ambayo inaweza kuwaunganisha kwa muda mrefu.
Amesema suala la kuungana kwa vyama vya kisiasa linahitaji zaidi ya mikutano ya viongozi na matamshi ya kisiasa, akisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa misingi na malengo yanayoeleweka kwa pande zote.
Kwa mujibu wa Rutto, tofauti za misimamo miongoni mwa viongozi wa upinzani zinaweza kuibua maswali kuhusu mwelekeo wa ushirikiano huo na kile wanacholenga kukifanikisha kupitia umoja wao.
APERIT FM,HII NI YETU

