Mfanyibiashara Oketch Salah ameshutumu vikali matapeli wa madini kwa kuharibu mazingira na miundombinu wakati wa utafutaji wa dhahabu kaunti ya pokot magharibi.
Akizungumza katika eneo la Lami Nyeusi wakati wa hafla ya ushirikishwaji wa umma kati ya kampuni yake, Tuyogh Gold Investors, na jamii ya eneo hilo, Salah amesema kwamba mashimo yaliyoachwa wazi na wachimba madini haramu ni hatari kwa usalama wa wakazi na pia mazingira kwani kuna watu waliopoteza maisha kutokana na mashimo hayo akiahidi kuwa shughuli zake za uchimbaji dhahabu zitaifaidi jamii akisema kwamba madini hayo yanaapaswa kuboresha maisha ya wenyeji ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara.