Wafanyibiashara katika mji wa Kabarnet kaunti ya Baringo wamepata hasara kubwa baada ya moto mkubwa kuzuka na kuharibu maduka na vibanda vyao na kusababisha uharibifu wa mali ya mamilioni ya pesa.
Wafanyabiashara walioathiriwa wameelezea masikitiko yao, wakisema moto huo umeteketeza kila kitu walichokuwa nacho.
Aidha wameitaka serikali ya kaunti na wafadhili mbalimbali kuingilia kati na kutoa usaidizi ili kuwasaidia kurejesha biashara zao ambazo wamezitegemea kama injini ya uchumi.