Mbunge wa Kibwezi Magharibi Mwengi Mutuse amewataka wakazi wa kaunti ya Pokot Magharibi kujitenga na viongozi wanaoeneza siasa za kikabila.
Mutuse, aliyezungumza katika kaunti ya Pokot Magharibi, amesema siasa za kikabila hazina nafasi katika jamii ya sasa, akisema zinashusha hadhi ya taifa na kuzuia nchi kusonga mbele kimaendeleo.
Aidha, mutuse amesema uongozi wa rais William Ruto umeleta mageuzi katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwemo katika uchumi na sekta ya elimu.
Ametumia fursa hiyo kuwarai wakazi wa kaunti ya hiyo kuhakikisha watoto wao wanapelekwa shuleni, akisisitiza umuhimu wa elimu katika kuandaa kizazi cha baadaye.
APERIT FM.HII NI YETU

