Mbunge wa Turkana Kaskazini, Ekwom Nabuin, ametoa wito kwa serikali kuzingatia usajili wa silaha zinazotwaliwa kutoka kwa jamii badala ya kuziondoa moja kwa moja, akionya kuwa hatua ya kuipokonya jamii silaha hizo bila kuweka mikakati mbadala inaweza kuzifanya kuwa katika hatari ya kushambuliwa.
Nabuin amesema ni muhimu serikali kutafuta mbinu za kukabiliana na changamoto za usalama zinazozingatia hali halisi ya maeneo yaliyoathiriwa na ukosefu wa usalama, hususan katika maeneo ya wafugaji ambako wananchi wamekuwa wakikabiliwa na vitisho vya mara kwa mara.
Amesisitiza kuwa usajili wa silaha hizo unaweza kusaidia katika kuimarisha usimamizi na uwajibikaji, huku serikali ikiendelea kutekeleza mikakati ya kurejesha amani na kuhakikisha usalama wa wananchi.Ametoa wito kwa serikali kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha jamii zinaendelea kulindwa dhidi ya mashambulizi na vitisho vya kiusalama.
APERIT FM,HII NI YETU

