Rais William Ruto, anatarajiwa kuondoka nchini juma lijalo kuhudhuria kongomano la baraza kuu la umoja wa mataifa unaofanyika Jijini New York, Marekani, akijiunga na viongozi kutoka mataifa mbalimbali duniani kwa ajili ya kujadili masuala muhimu yanayoikabili Jumuiya ya kimataifa.
Katibu wa maswala ya nchi za kigeni Kipkorir Sing’oe amesema Rais Ruto anatarajiwa kuwasilisha mtazamo wa kenya kuhusu masuala ya maendeleo, ushirikiano wa kimataifa na changamoto zinazohitaji juhudi za pamoja kutoka kwa mataifa mbalimbali.
Amesema miongoni mwa masuala yanayotarajiwa kupewa uzito katika mijadala ya kimataifa ni pamoja na maendeleo endelevu, mabadiliko ya tabianchi, amani na usalama, uchumi wa dunia, afya, ajira kwa vijana, pamoja na utekelezaji wa malengo ya maendeleo.
Rais Ruto pia anatarajiwa kutumia fursa hiyo kufanya mazungumzo na viongozi wengine wa dunia kuhusu masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, na kutia saini mikataba ya kibiashara
APERIT FM,HII NI YETU

