Wakulima wa mahindi kutoka kaunti ya Transnzoia, wanakadiria hasara kutokana na kuharibika kwa mazao shambani, wakiitaka bodi ya kitaifa ya nafaka na mazao NCPB, kufungua mashine ya kukausha nafaka, ili kuwaepushia hasara inayoshuhudiwa kutokana na mahindi kuoza.
Wakiongozwa na fredrick rono ambaye ni mkulima anasema magunia 30 kati ya 200 ambayo ameyavuna yameoza huku akiishinikiza serikali kununua mahindi gunia moja ya kilo 50, kwa shilingi elfu tatu wala sio efu tatu mia tano kwa kilo 90.
Rono anashinikiza serikali kupunguza bei ya mbolea ya kilo 50 kutoka shilingi 2500 hadi shilingi 1500, ili kupunguzia mkulima gharama ya uzalishaji na kupata faida.