Serikali imeahidi kupunguza mzigo wa kifedha kwa wazazi wa wanafunzi katika Chuo cha Mafunzo ya Matibabu cha Kenya (KMTC) ambao wametengwa kupata ufadhili wa elimu kutoka kwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELB).
Naibu Rais Kithure Kindiki ametoa tangazo hilo Alhamisi wakati wa hafla ya kuhitimu kwa wanafunzi wa KMTC katika Kituo cha Michezo cha Kimataifa cha Moi, Kasarani, ambapo wahitimu 22,776 walipokea cheti na diploma katika taaluma mbalimbali za afya.
Kindiki aliangazia shinikizo la kifedha linalowakabili wanafunzi hao akisisitiza kwamba mkopo wa HELB utasaidia kuhakikisha hakuna mwanafunzi atakayeachwa nyuma kimasomo.
Naibu Rais pia alipongeza mageuzi katika sekta ya afya nchini chini ya utawala wa Ruto katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita akitaja mafanikio ikiwa ni pamoja na usajili mkubwa wa Wakenya chini ya Mamlaka ya Afya ya Kijamii (SHA), ambayo imeboresha huduma ya matibabu kutoka milioni 7.5 mwaka wa 2022 hadi karibu milioni 28 leo.
Serikali pia imewaajiri Wahudumu wa Afya nyanjani 107,000,katika juhudi za kuboresha afya kwa wakenya