Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen ametangaza kukabiliana na wahuni wa kisiasa kote nchini kufuatia wimbi la ghasia zilizotatiza uchaguzi mdogo katika maeneo mbalimbali mnamo Alhamisi, Novemba 27, 2022.
Akizungumza wakati wa kufuzu kwa zaidi ya Machifu 6000 katika Chuo cha Kitaifa cha Polisi cha Embakasi jijini Nairobi, Murkomen amesema kwamba matukio haya hayatakubalika na watakaokamatwa watachukuliwa hatua za kisheria
Kadhalika Murkomen amebainisha kuwa machifu wamekuwa wakitatizika kusimamia hafla za umma, hata mazishi, kutokana wahuni wanaozua vurugu katika hafla hizo.