Maamlaka ya Afya ya Jamii SHA imetangaza kuwa, kuanzia sasa malipo kwa Zahanati na Hosipitali zinazotoa huduma za matibabu ya kawaida yatategemea kiwango cha dawa wanazowapa wagonjwa baada ya kuandikiwa.
Afisa mkuu mtendaji wa SHA Dkt Mercy Mwangangi, amesema baadhi ya zahanati na hosipitali hazijakuwa zinawapa wagonjwa dawa zozote wanazo stahili chini ya mpango wa huduma za afya unaofadhiliwa na maamlka hiyo ya SHA.
Kupitia mfumo wa kidijitali, SHA ilifuatilia dawa zilizo andikiwa wagonjwa na zile zilizotolewa.
Hosipitali au Zahanati zitakazo toa dawa zote zilizo andikiwa italipwa kikamilifu kwa dawa kuwa sehemu ya malipo ya dawa, uku ikiyatoa dawa chache ikilipwa kulingana na kiwango cha dawa ilizotoa.
SHA imesema mfumo huo inalenga kuhakikisha wagonjwa wanapata dawa zote walizo andikiwa na kuongeza uwajibikaji katika utoaji wa huduma za afya nchini.

