You are currently viewing SIGOR YALENGA WAPIGA KURA ALFU 60 KWENYE UCHAGUZI UJAO

SIGOR YALENGA WAPIGA KURA ALFU 60 KWENYE UCHAGUZI UJAO

Mbunge wa Sigor Peter Lochakapong amesema eneo bunge lake linalenga kuongeza idadi ya wapiga kura hadi alfu sitini kuelekea uchaguzi ujao 

Akizungumza katika eneo la Chepkondol Lochakapong amesema uwongozi wake umeendelea kuwahamasisha wananchi ambao hawana vitambulisho kutumia fursa iliyotolewa na serikali ili kupata stakabadhi hiyo muhimu

Aidha ametoa hakikisho kwamba wenyeji wa eneo hilo wanaunga mkono kwa asilimia mia moja kwa rais william ruto kuelekea uchaguzi ujao

Lochakapong amekariri haja ya serikali kuhakikisha barabara za mashinani zinakarabatiwa ili kurahisisha shughuli za usafiri huku akiweka wazi kwamba miradi kama vile uunganishaji wa umeme utaanza kufanikishwa hivi karibuni

APERIT FM,HII NI YETU