Waziri wa afya Aden Duale sasa ameendelea kusistiza kuwa hatafika mbele ya tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa NCIC kujibu tuhuma za matamshi ya uchochezi, iwapo aliyekuwa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua atakosa kuhojiwa na tume hiyo.
Akizungumza huko Garrisa, Duale amesema Gachagua ndiye anaye paswa kuwa wa kwanza kuchunguzwa kwa madai ya matamshi ya chuki, dhidi ya jamii ya Wasomali na Waislamu, akidai hajawai kuomba msamaha kwa kauli hizo.
Waziri Duale ameishtumu NCIC kwa kile anasema ni kutumia viwango tofauti kuwachunguza viongozi wanao tuhumiwa kwa matamshi ya chuki, akisema viongozi wa serikali ulengwa uku viongozi wa upinzani wakiwachwa bila kuchukuliwa hatua.
Pia amesisitiza kuwa hataomba radhi kwa matamshi aliyoyatoa akiwa mandera, akisema lengo lake lilikuwa la kuhamsisha jamii yake kuunga mkono serikali.

