You are currently viewing UHABA WA MAZIWA WAENDELEA NCHINI

UHABA WA MAZIWA WAENDELEA NCHINI

Uhaba wa maziwa umeendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini, kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa huku suluhu ya haraka ya kukabiliana na hali hiyo ikikosekana.

Uhaba huo umechochea kupanda kwa gharama ya vyakula vya mifugo , huku baadhi ya maduka makuu yakiweka kikomo kwa kiwango cha maziwa ambacho kila mteja anaruhusiwa kununua.

Hali hiyo imezua malalamiko kutoka kwa wakulima wa maziwa, ambao wanaulaumu serikali kwa kile wanachosema ni kupanda kwa gharama ya chakula cha mifugo.

Wakulima wanasema gharama kubwa ya uzalishaji imeathiri uwezo wao wa kuzalisha maziwa kwa kiwango kinachokidhi mahitaji ya soko.

APERIT FM,HII NI YETU