Serikali imezindua mpango wa kuwapa vijana fursa ya kufanya kazi katika mradi ujenzi wa nyumba za bei nafuu katika kaunti ya Turkana, hatua inayolenga kuwajengea ujuzi na kuwapa ajira kupitia mradi wa makazi unaotekelezwa na serikali.

Akizungumza mjini lodwar, Julius Kavita kamishna wa kaunti hiyo amesema kuwa mpango huo unahusisha mafunzo kwa vijana arobaini na moja waliohitimu na waliotuma maombi ya kazi, kabla ya kushiriki kwenye ujenzi wa nyumba hizo za bei nafuu, sehemu ya juhudi za serikali kuongeza ajira kwa vijana na kuboresha makazi nchini

Hii ni sehemu ya mpango mkubwa wa mradi wa nyumba za bei nafuu unaolenga kujenga makazi kwa gharama nafuu na pia kuleta ajira kwa vijana wa eneo hilo na mataifa mengine kote nchini.