Hali ya huzuni imetatanda katika kiji cha Kamelei katika eneo bunge la Pokot Kusini, kaunti ya Pokot Magharibi, hii ni baada ya wavulana watatu kufa maji katika bwawa la turkwel.
Kulingana na wakaazi wa eneo hilo, vijana hao walivuna na kuuza viazi vyao kisha kununua pikipiki ambayo walitumia kutembelea kwa mara ya kwanza.
Kulingana na benard abonyo,mkuu wa kituo cha turkwel, Safari yao kwa ajili ya kujivinjari iliwafikisha katika bwawa la turkwel ambapo waliamua kuogelea mmoja wao alianza kuonesha dalili za kuzama majini kabla ya wengine kuchukua hatua ya kumwokoa lakini baadae wakazama wote.
Abonyo ametoa wito kwa mamlaka ya kvda, kuajiri watu walio na ujuzi wa kuogelea ili kuwasaidia na kuwaelekeza wageni katika bwawa hilo la turkel. Miili yao imepatikana kando ya bwawa hilo ikielea kabla ya kupelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hosiptali ya rufaa ya kapenguria.