You are currently viewing WAKULIMA WEST POKOT WAHIMIZWA KUNUFAIKA NA MVUA ZA EL NIÑO

WAKULIMA WEST POKOT WAHIMIZWA KUNUFAIKA NA MVUA ZA EL NIÑO

Waziri wa Kilimo katika Kaunti ya West Pokot, Wilfred Long’uronyang, amewataka wakulima kutumia vyema mvua za El Niño zinazotarajiwa kunyesha ili kuongeza uzalishaji wa chakula na kujikinga dhidi ya baa la njaa linalotokana na kufeli kwa mazao msimu huu.

Akizungumza katika kikao kilichowakutanisha viongozi wa kaunti na wadau mbalimbali, Long’uronyang amesema wakulima wanapaswa kutumia fursa ya ruzuku inayotolewa na serikali, ikiwemo kupunguzwa kwa bei ya mbolea hadi shilingi 2,000, ili kuongeza uzalishaji wa chakula.

Aidha, waziri huyo amewataka wafugaji kupunguza idadi ya mifugo kutokana na upungufu wa malisho, ili kuepusha mizozo inayoweza kujitokeza kutokana na ushindani wa rasilimali.

Amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza hasara miongoni mwa wafugaji na kuongeza tija katika ufugaji.

APERIT FM,HII NI YETU