Mwakilishi wa kike kaunti ya Pokot Magharibi, Rael Aleutum, ameendesha hafla ya uzinduzi wa basari na sodo katika shule ya msingi ya tomena iliyoko eneo bunge la Kapenguria kaunti ya Pokot Magharibi.

Mwakilishi huyo wa kike amesema usambazaji wa sodo kwa watoto wa kike katika kaunti hiyo, pamoja na basari ya kima cha milioni 4.6, itawawezesha watoto kupata elimu, pamoja na fursa ya kipekee itakayo mfaa mtoto wa kaunti hii akiahidi kufanya maendeleo kwa shule ya msingi ya tomena pamoja na ya upili, huku akitoa ufadhili wa tenki ya maji kwa shulee hizo mbili .

aidha ameongeza kuwa basari hiyo ni kwa ajili ya kurahisisha elimu kwa watoto wote, kwani elimu ndio daraja pekee ya kuwakutanisha maskini na matajiri