You are currently viewing WAZIRI MURKOMEN AWAHIMIZA WAKENYA KUZINGATIA UTENDAKAZI WA VIONGOZI KUELEKEA UCHAGUZI UJAO

WAZIRI MURKOMEN AWAHIMIZA WAKENYA KUZINGATIA UTENDAKAZI WA VIONGOZI KUELEKEA UCHAGUZI UJAO

Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen, amesema viongozi ambao wamewahi kushikilia nyadhifa mbalimbali wanapaswa kwanza kuwasilisha rekodi ya utendaji wao kabla ya kupewa nafasi ya kuwania nyadhifa nyingine za kisiasa.

‎Murkomen amesema wapiga kura wanapaswa kuwatathmini viongozi kwa kuangalia kile walichofanikisha walipokuwa madarakani, badala ya kutegemea ahadi na kauli za kisiasa pekee. Kauli hiyo inakuja wakati wanasiasa wanaendelea kujipanga kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

‎Amesisitiza kuwa uongozi unapaswa kupimwa kupitia matokeo, uwajibikaji na huduma zilizotolewa kwa wananchi. Kwa mtazamo wake, viongozi wenye rekodi nzuri wanapaswa kuwa tayari kuieleza hadharani, huku wananchi wakipewa nafasi ya kuamua iwapo wanastahili kupewa mamlaka zaidi.