Viongozi wanaoegemea serikali, wametetea ziara za kila mara za wananchi katika ikulu wakisema, rais aliahidi kuwashugulika watu wote.

Msaidizi wa rais Faruok Kibet,amewakosoa wanaopinga ziara hizo akisema,ziara hizo zinasaidia katika kuwahusisha wahusika na kupata Suluhu.

Matamshi ya Faruok yanafuatia kauli ya aliyekuwa naibu rais aliyetimuliwa Rigathi Gachagua,ambaye alidai,ziara hizo huwa ni mbinu ya kuwahonga wakenya.

Wakizungumza waakati wa hafla ya kuwawezesha akina mama wa kaunti ya Pokot Magharibi eneo la Makutano,viongozi hao wamesema,raia anajitahidi kuwaunganisha wakenya wote.

Wakati huohuo,spika katika bunge la kitaifa Moses Wetangula,amesema serikali ya Kenya Kwanza inajitahidi kutekeleza ahadi walizotoa kwa wakenya.

Aidha,amesema,serikali imewaajiri walimu laki moja katika kipindi cha miaka mitatu sasa na kwamba,itaendelea kuwaajiri walimu zaidi nchini.

Wakati huohuo,Wetangula amewataka viongozi kutoka kaunti ya Pokot magharibi kutumia madini yanayopatikana katika eneo hilo ili kuinua maisha ya wakazi wa kaunti hiyo.