Hospitali za kibinafsi chini ya Muungano wa Hospitali za Kibinafsi za Vijijini na Mijini (RUPHA) zimetangaza kusimamisha huduma kwa wagonjwa kupitia mpango wa bima ya Mamlaka ya Afya ya Kijamii (SHA) hadi pale serikali itakamilisha deni la shilingi bilioni 10.6.
Hospitali hizo zimewataka wanaotafuta huduma za matibabu kulipa pesa taslimu kwa huduma katika vituo vyao vya afya.
Wakati serikali inapanga kuwapandisha walimu kwenye mfumo mpya wa matibabu wa maafisa wa umma ulioanzishwa chini ya SHA, hospitali za kibinafsi zimetishia kuacha kutoa huduma kwa watumishi wote wa umma.Serikali inapanga kuwaweka walimu kwenye mpango huo mpya baada ya kumalizika kwa bima yao ya sasa ya matibabu iliyotolewa na muungano unaoongozwa na Minet Kenya.