Na Jamin Ngeywo

Wahasiriwa wa dhulma katika eneo la Kapsiro iliyoko Mlima Elgon kaunti ya Bungoma wameripotiwa kutopata haki kutokana na uhafifu wa ushahidi unaowasilishwa katika mahakama.

Wazazi katika eneo hilo wametakiwa kukumbatia suala la kutoa ushahidi mahakamai ili kusaidia katika kupatikana kwa haki kwa aliyedhulumiwa.

Kulingana na washikadau eneo hilo,watu wengi waliodhulumiwa hawajapata haki kutokana na idadi kubwa ya wananchi kuhofu kutoa ushahidi katika kesi za dhulma mahakamai.

Wakizungumza eneo la Kopsiro,wakazi wamependekeza kujengwa kwa kituo cha uokoaji ambacho kitatumika kuwahifadhi watu wanaotoroka dhulma majumbani