Watu wanne wameripotiwa kufariki akiwemo mtoto wa miaka kumi na nne katika eneo la Kambi Karaya kaunti ya Pokot Magharibi baada ya kuporomoka kwa mgodi wakiendeleza shughuli ya uchimbaji madini
Kutokana na visa vya watu kupoteza maisha mara kwa mara kwenye migodi serikali iliweka hatua za ziada kukomesha uchimbaji haramu wa madini pokot magharibi na kaunti zingine, katika juhudi za kuzuia vifo zaidi vinavyohusiana na uchimbaji madini.
Miili ya wanne hao imepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Kapenguria.