Rais William Ruto amemteua John Cox Lorionokou kuwa msajili mkuu wa vyama vya kisiasa nchini.

Lorionokou ambaye ni mzaliwa wa kaunti ya Pokot Magharibi,atahudumu kwenye wadhifa huo kwa kipindi cha miaka sita ijayo.

Kuteuliwa kwake kunafuatia kuidhinishwa kwake na bunge la kitaifa lililompiga msasa kiongozi huyo

Viongozi wa kaunti ya Pokot Magharibi wanaendelea kutuma jumbe za heri njema kwa afisa huyo ambaye ameonekana kuiweka kaunti ya Pokot Magharibi kwenye ramani ya kitaifa