Rais William Ruto ametangaza mipango ya kuanzisha hazina mpya inayolenga akina mama wasio na waume na wanawake ili kusaidia kuwawezesha kiuchumi.

Akizungumza wakati wa ibada ya mazishi ya Weston Kanja, babake Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja,  huko Thome, Kaunti ya Laikipia, Rais Ruto amesema kuwa serikali itawafunza wanawake kupitia mipango ya serikali ya kitaifa na ya kaunti ili kuwasaidia kupata utaalam wa biashara.

Aidha Ruto ameeleza kuwa mpango huo mpya utaendana na mpango unaoendelea wa NYOTA, unaolenga kuinua makundi yaliyo katika mazingira magumu kote nchini kwa kutoa mafunzo, ushauri na upatikanaji wa fedha.