Kufuatia uchaguzi wa October 29, Samia Suluhu Hassan, ameapishwa rasmi kuwa rais wa taifa la tanzania, hafla hiyo ambayo imefanyika jijini dodoma, imehudhuriwa na viongozi mbalimbali, akiwamo naibu wa rais wa Kenya Prof Kithure Kindiki ambaye amemwakilisha rais William Ruto.

Katika kiapo hicho rais Suluhu ameapa kuilinda katiba ya nchi hiyo, na kuwaunganisha watanzania wote.

Hata hivyo, kuapishwa kwa Rais Suluhu kulifanyika huku mtandao bado ukizuiwa baada ya maandamano ya uchaguzi ambapo upinzani unasema mamia ya watu waliuawa na vikosi vya usalama.

Ushindi wake ulikataliwa vikali na chama kikuu cha upinzani, Chadema, ambacho kilizuiwa kushiriki, na kimeitisha uchaguzi mpya, kikiutaja kura ya uchaguzi ya Oktoba 29 kuwa ya uongo.

Tume ya uchaguzi inasema Hassan alishinda asilimia 98 ya kura.