Idadi ya watu ambao wamefariki dunia kutokana na mkasa wa maporomoko ya ardhi kwenye maeneo ya bonde la Kerio, pamoja na Kibendo kule Elgeiyo Marakwet, imefikia watu 32, katika kisa cha kwanza kwenye bonde la kerio miili minne ilipatikana jana, na kufikisha idadi jumla kuwa 32, kufuatia mkasa huo wa Jumamosi iliyopita.
Miili iyo nne inajumuisha moja ya mwanamme na tatu ya wanawake, aidha manusura bado wanatibiwa katika hosipitali ya rufaa ya Moi mjini Eldoret, baada ya kusafirishwa kwa ndege hadi Uasin Gishu.
Kwenye kisa cha pili kule Kibendo watu wengine wawili, walifariki dunia baada ya kusombwa na maporomoko ya ardhi juzi JumaPili.