Afisa wa madini katika kaunti ya Pokot Magharibi Brian Bundi, amewaonya wahisani ambao wanaendesha uchimbaji wa madini bila leseni kukoma na kufuata utaratibu unaofa ili wasije wakachukuliwa hatua kali za kisheria

Akizungumza na wanahabari, Bundi amesema kuwa tayari wamewakamata baadhi ya wahisani kumi wa uchina, ambao walikuwa wanaendesha shughuli hiyo ya uchimbaji wa madini bila leseni katika eneo la Kambi Karaya, Lami Nyeusi na Turkwel, kutokana na oparesheni iliyohusisha vitengo mbalimbali vya madini na usalama.

Bundi vilevile amesema kuwa, wamesitisha shughuli zote za uchimbaji wa madini katika maeneo mbalimbali katika kaunti hii ya Pokot Magharibi, ili kupiga msasa idadi ya wahisani ambao wanaendesha shugli hiyo ya uchimbaji madini