Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC inasimamia chaguzi ndogo katika maeneo 24 nchini huku wagombea 181 wakiwania viti tofauti tofauti.
Kati ya maeneo hayo yote,wadi ya Kariobangi Kaskazini katika eneo bunge la Embakasi kaunti ya Nairobi na wadi ya Chewani katika eneo bunge la Galole kaunti ya Tana River ndizo zina idadi kubwa ya wagombea .
Shuguli ya upigaji kura katika vituo mbalimbali ilianza mapema leo huku vituo kadhaa vikisajili idadi ya wastan ya wapiga kura.
Katika eneo bunge la Malava katika kaunti ya Kakamega,vurugu zilishuhudiwa ,mgombea wa ubunge kupitia chama cha DAP-K seth Panyako akidai kuwa,wahuni waliwamia na hata kumjeruhi dereva wake ambaye anadai amelaza katka hospitali ya rufaa ya Webuye
Katika eneo la Mbeere North,vurugu zilishuhudiwa huku aliyekuwa waziri Justin Muturi akikabiliana na agenti wa chama cha UDA Thuku Kiruga aliyekuwa amevalia sare za chama hicho
.