Kenya inakabiliana na ongezeko la kutisha la maambukizi mapya ya HIV, huku data mpya ikionyesha kwamba vizazi vya Gen Z na Milenia wanachangia idadi kubwa ya visa vipya, ikiashiria haja ya dharura ya kuweka mikakati inayolenga vijana ili kupunguza idadi hiyo.

Kwa mujibu wa Ripoti ya hivi punde ya Makadirio ya HIV iliyotolewa na Baraza la Kitaifa la Kudhibiti Magonjwa ya Sindemic (NSDCC) taifa limerekodi maambukizi mapya ya HIV 19,991 katika mwaka uliopita, kuashiria kupanda kwa asilimia 19 kutoka 16,752 mwaka uliopita.