Wakazi wa eneo bunge la Kapenguria, kaunti ya Pokot Magharibi, wanampongeza gavana Simon Kachapin kwa kuwateua maafisa wapya 16 katika wizara mbalimbali za kaunti. wizara hizo ni pamoja na kilimo, michezo, barabara, usafiri na miundombinu, pamoja na utalii na utamaduni.

Wakizungumza moja kwa moja na Aperit FM katika mji wa Makutano, wakazi hao wamesema wametambua hatua hiyo kama mwanzo mzuri wa kuimarisha utendakazi wa serikali ya kaunti, huku wakihimiza umakini zaidi hasa anapoendelea na hatamu yake ya uongozi.

Aidha, wamewataka maafisa hao wapya kutumikia wananchi kwa bidii katika idara walizopangiwa, wakidai kuwa baadhi ya mawaziri wa awali walikuwa wakilegea kazini na kushindwa kuleta maendeleo yaliyotarajiwa.

wakazi hao pia wamewahimiza viongozi wa kaunti kuzingatia uwezo wa watu wanaopewa majukumu, pamoja na kuhakikisha jinsia zote zinawakilishwa ipasavyo katika uteuzi wa nyadhifa mbalimbali.