Hali ya wasiwasi imetanda katika eneo la Ombolion,lokesheni ndogo Kases Pokot Kaskazini kwenye mpaka wa Pokot Magharibi na Turkana, baada ya mtu mmoja kupigwa risasi na kuuawa na watu wanaoshukiwa kuwa majambazi.
Kulingana na Chifu wa eneo la Ombolion Joseph Korkimul, marehemu, aliyetambuliwa kama Komole Siwa mwenye umri wa miaka 31 alipigwa risasi na kufa alipokuwa akichunga mifugo yake.
Korkimul ametoa wito kwa serikali kupeleka polisi zaidi katika eneo hilo, akitaja kuongezeka kwa mashambulizi ya ujambazi
Mtu mmoja aliuawa na watu wanaoshukiwa kuwa majambazi alipokuwa akichunga mifugo huko Ombolion, Pokot Kaskazini