Waziri wa fedha John Mbadi amekashifu viongozi wanaopinga mpango wa serikali wa kuuza asilimia 15 ya hisa za kampuni ya mawasiliano ya safaricom akisema viongozi hao hawana uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya biashara na uchumi.
Mbadi ameongeza kuwa hakuna kiongozi anayeweza kusimamisha mpango huo, akibainisha kuwa taratibu zote za kisheria za uuzaji wa hisa zinafuatwa.
Serikali imeanza kukusanya maoni ya wananchi kuhusu pendekezo hilo, ambalo limezua mjadala mkali nchini.