Kutokana na ongezeko la visa vya wizi hasa wanaowaibia watu baada ya kutoka benki na hata kwenye maduka kaunti ya Pokot Magharibi kamishna mpya wa kaunti hii David Saruni ametoa hakikisho la kukamatwa wahalifu hao

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya jamhuri katika shule ya msingi ya Makutano kamishna huyo amesema kwamba tayari mikakati imewekwa ili kuwanasa wahalifu hao na kuwawajibisha kisheria

Wakati huo uo Saruni ametoa onyo kwa wanaowalaghai wazazi kutuma hela ili wanao wapate nafasi ya kuajiriwa kwenye idara na tume za polisi akisisitiza kwamba mkono wa sheria ni mrefu huku akitoa wito kwa umma kushirikiana na polisi katika kuwakamata.

Hata hivyo Saruni amewataka madereva kuwa waangalifu na kuangazia kikamilifu sheria za trafiki ili kupunguza ajali za barabarani hasa msimu huu wa sherehe za krismasi na mwaka mpya.