Mtu mmoja amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Kapenguria katika kaunti ya Pokot Magharibi, kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea mapema leo katika barabara ya Kitale-Lodwar eneo la Bondeni.
Ajali hiyo ilihusisha gari la abiria la kampuni ya Great Rift na lori la kubeba mizigo lililokuwa likitoka upande wa Ortum kuelekea Kitale.
Aliyejeruhiwa ni dereva wa lori na kwa sasa anaendelea kupokea matibabu katika hospitali hiyo ya rufaa.
Wakazi wa eneo hilo wanadai kuwa,barabara hiyo ni finyu hali ambayo ilichangia kutokea kwa ajali hiyo na kuitaka Mamlaka ya Kitaifa ya Barabara Kuu nchini KeHNA kupanua Barabara hiyo.
Idara ya trafiki ya Polisi inatarajiwa kutoa maelezo zaidi kuhusu tukio hilo ambalo ni miongoni mwa matukio ya ajali katika Barabara kuu ya Lodwar-Kitale.
Ikumbukwe,jana Jumanne,basi lililokuwa safarini kutoka Isiolo kuelekea kwenye tamasha za Tobong’ulore katika kaunti ya Turkana lilihusika katika ajali enao la Kamatira huku watu wawili wakijeruhiwa vibaya.