Aliyekuwa mbunge wa Lugari Dr. Enoch Kibunguchy amefariki dunia mapema leo katika hospitali ya rufaa ya Eldoret baada ya kuugua kwa muda mfupi katika wiki mbili zilizopita.

Kwa mujibu wa familia yake, Dr. Kibunguchy alikuwa amelazwa katika hospitali hiyo baada ya kuugua kufuatia chakula alichokuwa amekila japo baadaye viungo vya mwili wake vilikataa kufanya kazi.

Famila yek inataka uchunguzi wa kina kufanywa kwa mwili wake ili kubaini chanzo cha kifo chake

Viongozi wa mrengo wa upinzani wanaitka usimamaizi wa hospitali hiyo kufanya uchunguzi na kutoa ripoti yao kwa familia hiyo.

Kifo chake kinajiri siku chache baada ya kifo cha Cyrus Jirongo,ambaye aliwahi kuhudum kama waziri na mbunge wa Lugari.