Rais Wiliam Ruto Ameongoza mkutano na mashirika pamoja na idara za serikali ili kuweka mikakati ya kupambana na matumizi mabaya ya pombe na dawa za kulevya kuambatana na ahadi zilizoainishwa katika Hotuba yake ya Mwaka Mpya akisema mfumo husika wa kisheria utakamilika ili kuimarisha uratibu na uwajibikaji kote serikalini huku maafisa wa ziada wakitumwa kwa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya.


Kadhalika Rais Ruto amesema vituo vya marekebisho vitazinduliwa katika kaunti zote 47, kwa ushirikiano na serikali za kaunti na vilevile NACADA, pamoja na kuimarishwa kwa huduma za ukarabati katika hospitali za rufaa na za kitaifa akiongeza kwamba Mamlaka ya Afya ya Jamii SHA itaimarisha bima ya matibabu .
Ili kukabiliana na ulanguzi wa dawa za kulevya na uhalifu , maafisa wa mpaka watatumwa katika vituo vitano muhimu vya kuingia humu nchini.


Wakati huo uo Ruto amesisitiza kuwa lengo bado liko wazi na serikali itatumia mbinu inayojumuisha serikali nzima ili kuzuia na kutekeleza matibabu kama njia moja ya kulinda wananchi pamoja na usalama wa taifa.