Jumla ya Wakenya 398 wamepoteza maisha kuanzia Januari 1, 2026 hadi Januari 30, 2026, na hivyo kuashiria wasiwasi mkubwa wa usalama barabarani nchini.
Kulingana na takwimu za Kitengo cha trafiki cha idara ya Polisi vifo hivyo vinawakilisha ongezeko la asilimia 11 ikilinganishwa na takwimu za mwaka jana.

Msemaji wa idara hiyo Boniface Otieno amebainisha kuwa jumla ya ajali 854 zilitokea barabarani, na kupita takwimu za mwaka jana za 850 zilizorekodiwa hadi mwisho wa mwaka. Kama matokeo, waathiriwa 2,032 walirekodiwa kufikia Januari 30, ikiwa ni ongezeko la asilimia 8 ikilinganishwa na 1,132 mwaka 2025.

Katika kipindi hicho, asilimia kubwa ya waliopoteza maisha ni wapita njia huku vifo 143 vikirekodiwa, wakifuatiwa na waendesha pikipiki 102.

Abiria walioaga dunia wakiwa 77, huku madereva 38 wakiangamia katika ajali mbalimbali zilizohusisha magari ya kibinafsi, mabasi na matatu na waendesha baiskeli 7 walikufa wakati wa siku 30