Kila mwaka Machi 4, ulimwengu huadhimisha Siku ya Unene Duniani ili kuangazia moja ya changamoto kubwa zaidi za afya ya umma katika enzi ya kisasa Daktari wa Hospitali ya Goodwill Cottage mjini kitale kaunty ya Trans Nzoia Maureen Mutua amelezea umihumu wa wananchi kuzingatia lishe bora ili kujiepusha na magonjwa kama shinikizo la damu,ugonjwa wa kisukari na magonjwa mengine.
Akizungumza hospitali humo Daktari mutua anaeleza hatari zinazotokana na unene kupita kiasi akielezea vyanzo vinavyosababisha unene kupitiliza nikama vile kutozingatia lishe bora na kutofanya mazoezi.
Hata hivyo Maureen pia ameelezea njia za kujikinga na unene kupita kiasi ni kufanya mazoezi na kuzingatia lishe bora.
Kulingana na Shirikisho la watu wenye Unene wa Kupindukia Duniani ya 2026, karibu watoto milioni 180 wenye umri wa miaka 5-19 walikuwa wakiishi na ugonjwa wa kunona sana mnamo 2025, na idadi hiyo inaweza kuongezeka hadi milioni 227 ifikapo 2040 ikiwa hatua kali hazitachukuliwa.
Wataalamu wa afya wanaona kuwa unene huongeza hatari ya magonjwa kama vile kisukari cha aina ya 2, magonjwa ya moyo na mishipa na baadhi ya saratani. Watoto walio na unene uliokithiri pia wana uwezekano mkubwa wa kubaki wanene wanapokuwa watu wazima, jambo ambalo huongeza hatari yao ya matatizo ya kiafya ya muda mrefu.