Gavana wa Tharaka Nithi, Onesmus Muthomi Njuki, ameteuliwa kuwa naibu Mwenyekiti mpya wa Baraza la Magavana (CoG).
Hii inafuatia kujiuzulu kwa Gavana wa Nyeri Mutahi Kahiga kutoka wadhifa huo mnamo Oktoba 22, baada ya kutoa matamshi yasiyojali kuhusu kifo cha Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga.
Njuki alikuwa akihudumu kama kiranja Mkuu wa baraza hilo tangu Oktoba 6, Hapo awali alikuwa mwenyekiti wa Kamati ya Afya ya katika baraza hilo.