Katika hatua za kuhakikisha elimu inaafikwa kikamilifu Kaunti ya Pokot Magharibi, gavana wa kaunti hii Simon Kachapin ametoa hakikisho la kuzinduliwa chuo kikuu kitakachoziba pengo la elimu

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya sherehe ya Mashujaa iliyofanyika katika shule ya msingi ya Makutano, gavana Kachapin amesema chuo cha awali cha Kisii kilichoko eneo la keringet kitafanyiwa marekebisho ili kuwa chuo kikuu na hili litanikishwa kupitia ushirikiano na chuo kikuu cha Nairobi na kuanza kutoa kozi mbalimbali ifikapo Septemba mwaka ujao

Kadhalika gavana Kachapin amewataka viongozi kutofanya siasa za mapema akisema kwamba wakati wa siasa utafika ambapo wananchi watawachagua viongozi wao