Gavana wa Uasin Gishu, jonathan bii, amependekeza jina la kaunti hiyo libadilishwe na kuitwa kaunti ya Eldoret. pendekezo hilo lengo lake ni kulinganisha jina la kaunti na jiji kuu la eldoret, kama ilivyo kwa kaunti nyingine zinazojulikana kwa majina ya miji yao mikuu, ikiwemo nairobi, kisumu, mombasa na nakuru.
Gavana Bii ametoa wazo hili alipohudhuria mkutano wa kwanza wa AI, akisisitiza kuwa jina la eldoret linajulikana zaidi na linaweza kutoa fursa mpya kwa kaunti.
Hata hivyo, baadhi ya wajumbe wamesema kuwa jina si tatizo kuu, bali serikali inapaswa kuzingatia maendeleo ya kaunti na kuboresha huduma kwa wananchi.
Gavana Bii amesema kuwa mapendekezo kama haya yanaweza kusaidia kaunti kukua kimaendeleo na kimfumo.