Kenya inakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi kutokana na kuongezeka kwa kiwango cha madeni, hali inayotishia udhabiti wa kifedha wa taifa.

Ripoti mpya ya shirika la okoa uchumi kuhusu madeni ya umma, imebainisha kuwa shilingi saba kati ya kila shilingi kumi zinazokusanywa na serikali zinatumika kulipa madeni, na kuwacha shilingi tatu pekee kwa matumizi mengine ya serikali, hii inahashiria kuwa nusu ya mapato ya taifa yanatumiwa kulipa madeni badala ya kutoa huduma muhimu kwa wananchi.

Kwa sasa jumla ya deni la taifa limefikia shilingi trilioni 11.81, ambapo deni la ndani ni shilingi trilioni 6.3 na deni la nje ni trilioni 5.48.

Hali hii imezua hofu miongoni mwa wananchi na mashirika ya kiraia mbayo yanadai kuwa madeni haya yamekuwa mzigo mkubwa kwa wananchi wa kawaida, ripoti hiyo imeelezea kuwa mikopo ya deni ya ndani imekuwa rahisi kufujwa, kwa kuwa haina ufuatiliaji mkali kama mikopo ya nje.